Jumatatu , 11th Jul , 2016

Tanzania imepokea Dola Milioni 200 kutoka Benki ya Dunia na umoja wa ulaya umetoa euro 180 kwa ajili ya kuwekeza katika mambo ya umeme nchini.

Tanzania imepokea Dola Milioni 200 kutoka Benki ya Dunia na umoja wa ulaya umetoa euro 180 kwa ajili ya kuwekeza katika mambo ya umeme nchini.

Hayo yamesemwa leo na waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati wa uzinduzi wa mpango wa Dunia wa nishati endelevu kwa wote,mradi wenye malengo ya ifikapo mwaka 2030 kila mwananchi awe ameunganishiwa nishati ya umeme hasa kwa jamii inayoishi vijijini.

Prof.Muhongo amesema sambamba na serikali kupata fedha hizo zauwekezaji unaenda sambamba na utengenezaji wa ajira nyingi nchini hasa kwa wazawa ambao ndio walengwa wakuu wa jambo hilo ili kutokomeza umaskini nchini.

Abasi Kitogo mtaalamu wa maswala ya nishati na mabadiliko ya tabia nchi kutoka umoja wa Ulaya amesema wameamua kuwekeza kwenye nishati ya umeme ili kuwasaidia watanzania walio maskini.