Jumatatu , 11th Apr , 2022

Mikoa ya Tanga na Dar es Salaam imetajwa  kuwa bado haijafanya vizuri kwenye zoezi la  uwekaji wa anuani za makazi kutokana na sababu mbalimbali huku mkoa wa Lindi na baadhi ya mikoa ya katikati ya nchi ikitajwa kufanya vizuri kwa asilimia 68 hadi 69.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akiwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza ziara maalumu ya ukaguzi wa zoezi la uwekaji anwani za makazi

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kabla yakuanza kwa ukaguzi maalum wa kuangalia zoezi la uwekaji anwani hizo kwa nchini nzima linavyoendelea kwa kutumia ndege maalum ya Jeshi, huku akitaja mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kuanza kukaguliwa.

EATV imepita baadhi ya maeneo ya Jijini la Dodoma kuangalia zoezi hilo linavyokwenda na kuzungumza na baadhi ya wananchi ambao walisema kipindi cha nyuma walikutana na changamoto yakuchagua majina ya mitaa lakini baada yakupewa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa majina na namba za mitaa yao ndipo walipokubali wenyewe kushiriki