Jumapili , 1st Jun , 2014

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, imewakamata watu watatu, wakiwamo wahandisi wawili wa manispaa ya Kinondoni, ambao wanatuhumiwa kutoa vibali vya ujenzi kinyume cha sheria.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU) Dkt Edward Hosea.

Taarifa zinadai waliokamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Kati ni mhandisi mkuu wa manispaa hiyo Bw. Baraka Mkuya, msaidizi wake aliyejulikana kwa jina moja la Christopher pamoja na mtendaji wa kata ya Msasani Bw. Gilbert Mushi.

Imedaiwa kuwa watendaji hao wa manispaa ya Kinondoni, walikamatwa juzi jioni kwa kudaiwa kutoa kibali cha ujenzi wa taa katika eneo maarufu kwa starehe la Coco Beach, ambapo baada ya kufuatiliwa ilidaiwa kuwa kibali hicho kilitolewa bila idhini ya uongozi wa manispaa ya Kinondoni.