Tuhuma ambazo zilikuwa zinawakabili ni kutokuwasilisha fedha ambazo ni mapato ya Serikali yaliyokusanywa kwa mfumo wa POS na kuzitumia kwa manufaa yao pasipo kuwasilishwa sehemu husika kwa taratibu zilizowekwa.
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Ramadhani Ndwatah ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia mwezi Octoba hadi Desemba mwaka 2024.
Ndwatah amesema kwamba baada ya kufikishwa mahakamani Jamuhuri ilishinda kesi hiyo ambapo watumishi hao waliamriwa na mahakama kurejesha fedha kiasi hicho kwa mchanganuo mbalimbali.
Aidha alisema kwa wilaya ya Kilindi katika ufuatiliaji wa Jamhuri kushinda kesi za kuhujumu uchumi namba 13,2023,11/2023 na 06/2024 dhidi ya watumishi ambao walishtakiwa kwa ubadhirifu kufuatia kutokuwasilisha fedha ambazo ni mapato ya Serikali yaliyokusanywa kwa mfumo wa POS na kuzitumia kwa manufaa yao pasipo kuwasilishwa sehemu husika kwa taratibu zilizowekwa.
“Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 58,678,780.00 zilirejeshwa na watumishi hao kwa amri ya mahakama sambamba na adhabu nyengine “Alisema #EastAfricaTV