Alhamisi , 14th Aug , 2014

Chama cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani TABOA, kimesema kimesikitishwa na mchakato wa kuhamishwa kwa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungojijini Dar es salam baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi DART.

Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi. Hawa Ghasia. Wizara yake inahusika na kituo kikuu cha mabasi Ubungo.

Akizungumza jana jijini Dar es salaam katibu mkuu wa TABOA, Ernea Mrutu amesema anasikitishwa kwa jinsi walivyotelekezwa kwa sababu hakuna wanaolifahamu juu ya maendeleo ya mchakato huo.

Mrutu amesema kuwa anafahamu Mradi wa DART kwenye kituo cha Ubungo unakaribia kukamilika lakini hakuna kilichofanyika kwenye maeneo ambayo yalitajwa kuwa yatakuwa na vituo mbadala hali inayotia shaka juu ya mustakabali wa biashara ya mabasi ya mikoani.

Wakati huo huo, kituo maalumu cha uendelezaji wa kilimo ukanda wa kusini mwa Tanzania SAGOT kimetoa wito kwa wakulima wadogo kuungana kwa kuunda vikundi vidogo ili kuirahisishia serikali kuwafikishia huduma muhimu za pembejeo na mikopo katika kuinua sekta hiyo nchini.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Ofisa mtendaji mkuu wa kituo hicho Geofrey Kirenga wakati akielezea mada atakazo ziwasilisha kwenye mkutano wa wadau wa umoja wa watendaji wakuu wa makampuni CEORT.

Aidha Dk Kayanda ametoa wito kwa makampuni binafsi kuwekeza kwenye sekta ya kilimo katika ukanda wa kusini kwa kuwa ni ukanda ambao hali yake ya hewa ni inayostawisha vyema mazao ya baishara na chakula.