Ijumaa , 14th Aug , 2020

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimesisitiza umuhimu wa kupatiwa elimu ya kutosha kwanza kabla ya kuanza kwa zoezi la abiria kukata tiketi kwa kutumia mfumo wa mtandao.

Msemaji wa Taboa Mustapha Mwalongo amesema zoezi hilo lilipaswa lianze mwanzoni mwa mwezi huu kama serikali ilivyowaagiza lakini wamiliki wa mabasi hawana elimu ya kutosha juu ya mfumo huo ikiwemo namna serikali itakavyopata mapato..

Amesema kutokana na kuchelewa kuanza kwa zoezi hilo TABOA imeitisha mkutano wa pamoja na kuishirikisha serikali katika mkutano huo utakaofanyika tarehe 22 mwezi huu ili kuto tamko la pamoja juu ya kuanza kwa zoezi hilo..

Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba kuanza kutumika mfumo wa ukataji tiketi kwa njia ya mtandao kutasaidia kuhibiti upotevu wa fedha za wamiliki wa mabasi, upotevu wa mapato ya serikali pamoja na kuondoa kero kwa abiria na udanganyifu.