
Bw. Wickremesinghe ana kazi kubwa ya kuiongoza nchi hiyo kuondokana na hali mbaya ya uchumi mbaya kuwahi kutokea na kurejesha utulivu wa jamii baada ya sintofahamu ya miezi kadhaa ya maandamano.
Amemshinda mshidani wake Dullus Alahapperuma, baada ya kupata kura 134 dhidi ya 82 za bunge la nchi hiyo .
Rais wa zamani wa Taifa hilo Gotabaya Rajapaksa aliikimbia nchi hiyo wiki iliyopita, ambapo anasemekana kukimbilia nchini Singapore baada ya meelfu ya waandamanaji kuvamia makazi yake na kuchoma moto ikiwemo pia majengo mengine ya serikali wakitaka ajiuzulu.