Meneja wa shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mkoa wa Arusha James Kisarika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Arusha James Kisarika, amesema kuwa kwa sasa wanashirikiana na Halmaashauri ya jiji la Arusha katika uanzishwaji wa mji mpya wa kisasa wa Safari city katika eneo la Mateves ambao uitabadili muonekano wa jiji la Arusha na kulifanya kuwa jiji la kimataifa.
Kisarika amesema kuwa tayari viwanja zaidi ya 600 vitauzwa katika eneo hilo kwa ajili ya uendelezaji wa nyumba za makazi za watu wa kipato cha chini,kati na cha juu ambapo wanunuzi watapatiwa ramani ya nyumba wanazopaswa kujenga ili kufanikisha ndoto za ujenzi wa mji huo mpya.
Afisa Mauzo wa shirika hilo Gibson Mwaigomole, amesema kuwa katika uuzaji wa viwanja hivyo hakutakua na madalali hivyo amewataka Watanzania kufika moja kwa moja katika ofisi za shirika hilo zilizoko katika kila kona ya nchi.
Mwananchi mmoja aliyepata eneo katika mji huo Thomas Kilaga mpya ameeleza kuwa amepata fursa ya kumiliki ardhi ambazo hazina migogoro ukilinganisha na ardhi nyingine