Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Khamisi Kigwangala.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe, Khamisi Kigwangala amesema kuwa sheria hizo ni ile ya mtu kufikia miaka 18 ni mtu mzima na ile isemayo umri wa msichana kuolewa ni miaka 15.
Dkt. Kigwangala amesema kuwa baadhi ya kazi ambazo zimeanza kufanywa ni pamoja na wizara ya katiba na sheria ya kuandaa waraka wa serikali kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho hayo.
Amesema kwa sasa waraka huo upo katika ngazi ya baraza la mawaziri kwa ajili ya kutolewa maamuzi na punde utakapokamilikaa taarifa itatolewa lakini mpaka sasa serikali imeshatunga sheria ya mtoto na kuweka tafsri moja kuwa mtoto ni chini ya umri wa miaka 18.