
Ngonyani ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze juu ya manufaa yaliyopatikana tangu sheria hiyo ianze kutumika.
''Sheria hii imesaidia sana mwanzoni kulikuwa na visa vilivoripotiwa polisi 459 ila baada ya kuanza kutumika kwa sheria hiyo kesi zimepungua sana mfano kesi za uchochezi zilizoripotiwa ni nne, kesi ya moja ya kutoa taarifa zisizo sahihi, tukio moja tuu la video ya ngono jambo ambalo ni hatua kubwa ukilinganisha na hapo awali''-Amesema Ngonyani
Aidha Naibu Waziri amewataka wananchi watakapoona wamedhalilishwa kupitia mitandao ya kijamiii mara moja waripoti vituo vya polisi ili uchunguzi na kubaini wahusika uweze kufanyika mara moja.