Jumatatu , 31st Aug , 2015

Serikali imesema kuwa sheria ya Makosa ya Mitandaoni na sheria ya Miamala ya kielectroni ya mwaka 2015 itaanza kutumika rasmi kesho na kuwataka wananchi wote kuzingatia matumizi sahihi ya Mitandao na vifaa vya Tehama.

Waziri wa sayansi na teknolojia prof Makame Mbarawa

Tamko hilo limetolewa leo jijin Dar es salaam na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa shria hiyo.

Mbarawa amesema kuwa matumizi sahihi ya Teknolojia yatailetea nchi Maendeleo na nchi nyingi zilizoendelea duniani zina sheria kama hizo ili kudhibiti uhalifu wa mitandaoni hasa kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na Teknolojia,

Profesa Mbarawa ameongeza kuwa sheria hiyo haijaja kuminya uhuru wa watu kutoa maoni na uhuru wa habari bali kudhibiti maudhui ya Uongo, wizi wa mitandaoni, Udanganyifu, kugushi, Picha chafu, Matusi na matumizi mabaya ya Vifaa vya kielectroniki.