Ijumaa , 2nd Aug , 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe ametembelea Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 leo Agosti 2, 2024 ambayo Kitaifa yanafanyika kwenye uwanja wa Nzuguni, jijini Dodoma.

Prof. Shemdoe ameambatana na viongozi na wataalamu wa Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Jabil Shekimweli na kutembelea maeneo mbalimbali yakiwemo vipando vya mahindi, vitunguu, alizeti na mtama.

Maonesho haya yenye hadhi ya Kimataifa yalizinduliwa Agosti 01, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kuhudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Kilimo; Wizara ya  Mifugo na Uvuvi  pamoja na Viongozi wa Mikoa, Wilaya, Taasisi mbalimbali Binafsi na za Umma; ikiwa ni pamoja na washiriki kutoka nje ya nchi.