
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adolf Mkenda
Akiongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam, katika mkutano wa kimataifa wa kuangazia mageuzi ya viwanda,iliyoandaliwa na ndaki ya sayansi za jamii chuo kikuu cha Dar es salaa.
Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Adolf Mkenda amesema ni lazima taasisi na mashirika yote yanayosimamia vibali, leseni, malipo na vigezo kwa wawekezaji kuunda chombo kimoja ili kuondoa kero na vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
Amesema, Kitendo cha mamlaka ya chakula na dawa TFDA pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mashirika na taasisi nyingine zinazosimamia usajili kutoungana ni miongoni mwa kero kubwa na chanzo kinachowakimbiza wawekezaji wengi na kuepelea wafanyabiashara kushindwa kurasimisha kazi zao na kupelekea serikali kukosa mapato kwawatu kuendesha shuguli zao kinyume na taratibu.
Adolf Mkenda amesema, mbali na mpango wa kuondoa vikwazo hivyo, serikali iko mbioni kuhakikisha kuwa miundombinu ya usafirishaji kwa njia ya reli, barabara na bandari inaimarika maradufu, upatikanaji wa maji ya uhakika na umeme wa bei nafuu ili kuchochea uzalishaji wa viwanda na uzalishaji kwa mazingira rahisi.