Jumanne , 2nd Feb , 2016

Serikali imekiri kuwa kasoro nyingi zilizojitokeza katika mradi Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ikimwo ubadhirifu wa fedha kwa Kaya sizizokuwa na sifa kupewa pesa kupitia mpango huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Angela Kairuki

Akijibu Swali la Mbunge wa Kaliua, Mhe. Magdalena Sakaya ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angela Kairuki ameitaka jamii kutoa ushirikiano kuwabaini wanaojinufaisha na mpango huo.

Mhe. Kairiuki amesema tatizo kubwa lililopo ni kutokana na vijana waliopewa jukumu la kuchukua madodoso katika kuzitambua kaya masikini ambapo wamekuwa wakiandikisha hata kaya ambazo hazina sifa na kusema kuwa atakayebainika basi serikali itachukua hatua.

Aidha amewataka wanakijiji wahudhurie mikutano inayoitishwa na pia wanapoona kuna kaya ambayo imeorodheshwa na haina sifa basi kupitia mikutano hiyo waweze kuchukua hatua za hapo hapo.

Pia waziri huyo amesema kuwa wananchi wengi wanaogopa kujitokeza katika kuchukua fedha hizo kwa kusikiliza maneno ya baadhi ya watu wanaodai fedha hizo ni za "Freemason" huku akisema fedha hizo zimetolewa na serikali katika kusaidia kaya hizo masikini.