Jumatatu , 2nd Aug , 2021

Serikali imeahidi kuendelea kutoa ajira mpya katika kada ya elimu ili kuziba pengo  kwa shule za msingi na sekondari ambazo bado zinakabiliwa na uhaba pamoja na upungufu wa walimu nchini.

Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde, wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ipinda wilayani Kyela  mkoani Mbeya wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema hadi sasa zaidi ya walimu 30 wa shule za msingi wilayani Kyela wameajiriwa na kwamba wataendelea kuajiri walimu ili kukabiliana na uhaba wa walimu huku akiwaahidi wananchi kwamba serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya elimu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kyela, Ally Mlaghila, amesema wilaya hiyo ina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi.