Alhamisi , 22nd Mei , 2014

Wizara ya Ujenzi imepanga kujenga barabara 41 na madaraja 13 nchini kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Kilomita 3,074, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa barabara ya Dar-es-salaam - Chalinze yenye urefu wa kilomita 100 kwa mwaka 2014/2015.

Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli akiwasislisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/2015, alisema ujenzi wa barabara na madaraja hayo utagharamiwa na serikali pamoja na wahisani.

Alisema baadhi ya barabara zilishaanza ujenzi na nyingine ndiyo zitaanza huku madaraja yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi na mengine yakihitaji upanuzi. Barabara za mikoa zitakazokarabatiwa ni za kilomita 685 za changarawe na za lami kilomita 78.