Alhamisi , 7th Apr , 2016

Serikali ya Tanzania imesema haina mpango wowote wa kutaifisha viwanda visivyofanya vizuri na ambavyo wamepatiwa wawekezaji kupitia utaratibu wa uwekezaji.

Waziri wa Viwanda na Biashara mhe. Charles Mwijage

Badala yake serikali imesema inakamilisha taratibu ili viwanda hivyo wapatiwe watu wenye uwezo wa kuviendesha kwa tija kuliko hali ilivyo hivi sasa.

Waziri wa Viwanda na Biashara mhe. Charles Mwijage amesema hayo katika kongamano la kimataifa la utafiti lililoandaliwa na taasisi ya utafiti wa kupunguza umaskini REPOA, ambapo mada kuu ni jinsi ya kufikia ndoto ya uchumi wa viwanda.

Kwa mujibu wa Waziri Mwijage, takribani viwanda arobaini vimeabinika kufanya vibaya na ambavyo serikali itapitia upya umiliki wake ili kuwapa wenye uwezo wa kuviendesha

Mhe Mwijage amefafanua kuwa malengo ya kubinafsisha viwanda hivyo ilikuwa ni kuongeza fursa za ajira, upatikanaji wa bidhaa pamoja na kuongeza mchango wa viwanda katika pato la taifa na sio kama ahli ilivyo sasa.