Jumatano , 25th Mei , 2016

Serikali imesema imetoa mafunzo ya kwa walimu elfu 22 mia sita 97 kwa stadi za kusoma kuandika na kuhesabu ikiwa ni katika kujenga mazingira mazuri kwa mwalimu na kuondoa tatizo la wanafunzi kumaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma na kuandika.

Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.

Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amesema serikali inatambua changamoto hiyo ndio maana wameamua kutoa mafunzo zaidi kwa wahusika wa elimu ili kupunguza kama si kuondoa kabisa tatizo hilo.

Prof. Ndalichako amesema serikali kwa sasa imeandaa na kusambaza vitubu katika kumirisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu huku serikali ikiendelea kutoa uhamsishaji kwa wazazi watambue wajibu wao katika maendeleo ya mtoto katika kupata elimu iliyobora.

Aidha, Waziri huyo wa Elimu amesema serikali imeandaa mpango maalumu wa kuwatambua walimu wa darasa la kwanza na li pili watakaofanya vizuri ili kuwapa motisha ya kuendelea katika kuwajengea misingi mizuri wanafunzi kuanzia ngazi ya chini.