
Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Akihutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kitaifa yaliyofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam,rais amesema serikali itaendelea kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wake kulingana na makusanyo ya mapato ya taifa.
Pia Rais Kikwete amesema serikali inafanya juhudi za kupunguza makato ya kodi kwa watumishi wa umma kutoka asilimia 13 ya sasa mpaka kufikia asilimia tisa.