Jumamosi , 8th Aug , 2015

Wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali wamesema kuwa kufuatia kuendelezwa kwa bandari ya Tanga kuendelea kufanya kazi kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo shughuli za usafirishaji wa kemikali ambazo ni hatari kutokaTanzania kwenda nje ya nchi.

Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akizungumza kwenye hafla.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa serikali Prof, Samweli V. Manyele wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa ambapo amesema

Wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali nchini moja ya kazi wanazozifanya ni pamoja na kudhibiti kemikali zitumikazo migodini, kujibu hoja za jamii na kulisaidia jeshi la polisi.

Aidha ameongeza kuwa wanategemea uwepo wao mkoani hapa utahakikisha na kusaidia wanachi wa Tanga pamoja na watumiaji wa barabara za kwenda mikoani zitakua salama ili kuepusha ajali zitakazoweza kutokea kutokana na kemikali mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa sayansi ya makosa ya jinai Gloria Omari amesema lengo la kutoa mafunzo ya jinai ni kutoa elimu ya majanga mbalimbali yatokanayo na kemikali haswa katika kuongezeka kwa viwanda na pia wananchi kuweza kutambua na kujikinga na kemikali hizo.