Alhamisi , 20th Aug , 2015

Mfuko wa Sekta binafsi nchini Umesema kuwa ili nchi ipate maendeleo endelevu ni lazima Serikali iweke kipaumbele katika Elimu ya ujuzi ambayo ndio chachu ya ufanisi katika shughuli za kujenga uchumi.

Mwenyekiti wa TPSF ambae pia ni mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP Dkt. Reginald Mengi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa TPSF Dkt. Reginald Mengi katika mkutano wa Pamoja kati ya wadau wa sekta binafsi na Serikali wa kujadili Sera ya maendeleo ya sekta binafsi hapa nchini na kuongeza kuwa hakuna nchi iliyofanikiwa bila kuwekeza katika Elimu hasa ya Ujuzi na kumtaka Rais ajae kipaumbele chake kikuu kiwe Elimu.

Aidha Dr. Mengi amesema kuwa kikwazo kikubwa cha Maendeleo hapa nchini ni Rushwa ambayo huwanyima watu haki na huduma muhimu za kijamii.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Msaidizi toka Ofisi ya Waziri Mkuu Ezamo Maponde amesema rushwa haikubaliki hapa nchini na kusisitiza kuwa watashirikiana na Sekta binafsi ili kupata Sera nzuri ya Maendeleo ya Sekta binafsi kwa Maendeleo ya nchi.