Akizungumza mara baada ya kukagua na kupokea taarifa ya maendeleo ya uboreshaji wa uwanja wa ndege jijini Tanga Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, amesema kuwa serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeamua kufanya maboresho makubwa kwenye viwanja vyote nchi nzima.
"Tunawaomba sekta binafsi watusaidie kuja kuingia kuwekeza katika sekta hii nunueni ndege za kutosha kwa sababu Air Tanzania peke yake haiwezi kununua ndege kwenye viwanja vyote nchini kwa mfano hivi tunavyozungumza kuna maombi ya kuongeza ndege Mbeya, Songea, Tabora, Mpanda na Rukwa," alibainisha Kihenzile.
Yusufu Zuberi Sood ni Meneja uwanja wa ndege Tanga amesema mara baada ya kukamilika kwa mradi wa maboresho katika uwanja huo utawezesha ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria 80 kutua jijini humo tofauti na sasa ndege ndogo ndio zinazotua.