Jumanne , 17th Mei , 2016

Serikali imesema haijanufaika na uuzwaji wa magogo na mbao nje ya nchi kwa muda mrefu kutokanana na biashara hiyo kufanyika kinyume cha sheria kwa muda mrefu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ramo Makani.

Akizungumza jana Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ramo Makani amesema katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 jumla ya fedha zilizopatikana kutokana na mauzi ya mbao nje ya nchi ni shilingi bilioni 269.

Mhe. Makani amesema kwa mujibu wa sheria na kanuni za misitu inakataza usafarishaji wa Magogo kwenda nje ya nchi na kununi hizo haziruhusu uzaji wa mbao nje ya nchi zenye unene usiozidi nchi sita.

Aidha, Mhe. Makani ameongeza kuwa Kanuni na Sheria hizo zinaweka zuio ili kutoa fursa ya kukuza viwanda vya ndani ya nchi na ajira kwa Watanzania katika kupasua mbao na utengenezaji wa samani.