Alhamisi , 14th Mei , 2015

Serikali imetakiwa kuiboresha sera ya elimu iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo inaeleza lugha ya kufundishia kuwa ni kishwahili ambapo imebanishwa kuwa kwa kufanya hivyo kutadumaza elimu nchini na kurudisha nyuma maendeleo.

Mbunge wa Urambo Magharibi Prof. Juma Kapuya .

Akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu leo Mbunge wa Urambo Magharibi Prof. Juma Kapuya amesema sera ya elimu ya ambayo imeweka lugha ya kufindisha kuwa kiswahili itajenga matabaka na itashindwa kuwajenga vijana katika kupambana na soko la Ajira hasa kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mh. Kapuya ameongeza kuwa viongozi wengi wanawapeleka watoto wao kwenye shule zenye mitaala ya Kiingereza hivyo kutawafanya watoto wengi wa masikini washindwe kupata kazi na huku akibainisha kuwa nchi nyingi zimepiga hatua kutokana na kuboresha mitaala yao ya kufundishia kwa kutumia ya Kiingereza.

Akitolea mfano nchi ya Indonesia ambayo wanatumia mitaala yao kwa lugha ya kingereza wamefanikiwa kupata mafanikio makubwa na kubadilisha teknolojia na kwa sasa wataalamu wengi wa sayansi wanatokea huko.

Aidha Mh. Kapuya amesema changamoto kubwa zaidi itakuwa kila soko la ajira kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo Kenya, Uganda na Rwanda ni nchi ambazo zimetoa kipaumbele katika somo la kingereza ili kufanikisha kutatua soko la ajira katika nchi hizo.