Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi nchini Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema lengo ni kuboresha mazingira ya kurahisisha ulipaji kodi kwa kuunganisha kodi zote za kampuni ndogondogo ili kuondoa usumbufu wa kukusanya kodi kwa kampuni mojamoja.
Amesema, kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMi), wamekaa na kujadiliana namna ya kutatua malalamiko ya wafanyabishara hapa nchini kwa lengo la kuondoa migogoro ya mara kwa mara.
Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara kuachana na dhana ya migomo kama kukomoana na serikali na badala yake watumie viongozi wao kuandaa hoja na kuzifikisha serikali ili kutafutiwa ufumbuzi.