Ijumaa , 3rd Jun , 2016

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ing. Ramo Makani amesema kwamba sekta ya utalii nchini imeendelea kufanya vyema katika nyanja tofauti ikiwemo ajira, pato la taifa na kuingiza asilimia 25 ya fedha za kigeni nchini.

Makani ameyasema hayo Bungeni alipokuwa akijibu maswali ya wabunge kuhusu wizara hiyo hususani maendeleo yake na fidia kwa askari wa wanyamapori wanaoumia kazini.

''Sekta ya utalii imeendelea kufanya vyema ambapo kwa miaka mitano mfulilizo imeweza kuongoza kwa kuingiza asilimia 25% ya fedha za kigeni, 17 % ya pato la taifa na 11% ya ajira nchini.

Aidha kuhusu kufidiwa kwa askari wanaoiumia kazini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama amesema kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu itaanza mwaka huu kushughulikia sheria inayotaka waajiri kuchangia mifuko ya fidia kwa wafanyakazi wao ili ikitokea ajali kazini mfanyakazi amepata ajali aweze kupatiwa fidia.