Sayansi yasaidia kukamata wahalifu
Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Mwamini Rwantale ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asili Jeshi la Polisi nchini kwenye hafla ya maadhimisho ya Sayansi jinai yaliyofanyika Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.
"Tumeshuhudia wahalifu wakikamatwa kirahisi na kuunganishwa na makosa yao waliyofanya huku wasio na hatia wakiachiwa huru mnaweza kuona ni kwa kiasi gani watuhumiwa walitiwa hatiani na wasio na hatia wakiachiwa huru", alisema Dcp Mwamini Rwantale, Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asili Jeshi la Polisi.
Aidha Rwantale anaelezea namna ambavyo wanafanikisha zoezi hilo.
"Pale linapouja swala la utafutaji haki, kila kitu kwenye eneo la tukio, unywele mmoja hata ikiwa tone la damu, muandiko kwenye karatasi vyote muhimu sana katika kubaini ukweli huadhimishwaji wa siku hii huadhimisha kwa matamasha mbalimbali na kuonesha umuhimu wa tasnia hii", alisema Dcp Mwamini Rwantale, Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asili Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, DCP. Lazaro Mambosasa anaelezea wanavyovumbua wahalifu.
"Tunachunguza ili kutoa haki, kwa sababu usipochunguza unaweza ukajikuta unamuingiza mtu kwenye hatia, lakini uchunguzi hauwezi kumuingiza asiye na hatia kwenye hatia na mara nyingi wanasema usipofanya utafiti huna sababu ya kusema lakini nyie mnatubeba kwakuwa mnafanya kazi kazi nzuri salama na isiyokuwa na wasiwasi", alisema Dcp. Lazaro Mambosasa -Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
"Ni chnguzi ambazo zinatoa uhakika wa jambo ili kurahisisha maamuzi ya kisheria klwenye mihimili inayohusika na kutoa haki, sasa umuhimu wa Sayansi hii kwenye jamii yetu ni kutoa haki kwa njia ya kisasa zaidi", alisema Fidelis Sekumb, Ofisa kutoka Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa serikali.