Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto nchini Tanzania imesema magonjwa ya saratani yamekuwa yakiongezeka nchini ambapo wagonjwa wapya 44,000 hugundulika kuwa na saratani za aina mbalimbali kila mwaka kutokana na kuchelewa kugundulika mapema.
Takwimu za Shirika la kimataifa la Atomic la utafiti wa Saratani IARC na Shirika la afya Duniani WHO kila mwaka kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milion 14.1 kati yao zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na kuchelewa kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Ulusubisya anasema miongoni mwa saratani zinazosababisha vifo nchini ni pamoja na saratani za ngozi, koo na tezi dume kwa upande wa wanaume na saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti.
Kufuatia hali hiyo wizara ya afya inawataka wananchi kuchukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kupima afya zao mara waonapo dalili za awali kutokana na saratani kusababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uvutaji wa sigara na unywaji pombe.


