Ijumaa , 10th Jun , 2022

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani katika kesi ya uhujumu uchumi.

Lengai Ole Sabaya

Hukumu hiyo imetolewa leo Juni 10, 2022, na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo,Patricia Kisinda, na kusema kuwa mbali na sababu hizo, Mahakama imegundua kuwa hati ya mashtaka ilikuwa na mapungufu na kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yao mahakamani hapo haujaweza kuthibitisha mashtaka hayo.

Hii ni kesi ya pili Sabaya kushinda ambapo Mei 6, 2022 na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura,walishinda rufaa iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, waliyokata kupinga hukumu ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.