Mchumi mkuu katika Wizara ya Fedha ya Rwanda Leonard Rugwabiza.
Hatua hizo ni sehemu ya mapendekezo ya ripoti ya Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyozinduliwa mjini Nairobi, Kenya mwezi uliopita
Mchumi mkuu katika Wizara ya Fedha ya Rwanda Leonard Rugwabiza, amesema hatua moja wapo watakayochukua ni pamoja na kuomba huduma za utumaji fedha nchini humo kupunguza gharama za upokeaji wa fedha kutoka kwa Wanyarwanda waishio nje ya nchi.
Bw. Rugwabiza, amesema idadi ya wanyarwanda walioko ughaibuni ni ndogo lakini pia watapunguza kodi ya kuchukua fedha kutoka kwa nchi za afrika mashariki ili kupata wengi zaidi ambao watakuwa wanatuma pesa nchini humo
UNCTAD inasema zaidi ya dola Bilioni 600 zinahitajika kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu na hilo linawezekana iwapo nchi zitategemea zaidi vyanzo vya ndani vya mapato badala ya mikopo na misaada ya maendeleo.