Jumatano , 12th Nov , 2014

Mwenyekiti wa bodi ya TPSF Dkt. Reginald Mengi amesema kumekuwa na changamoto nyingi kwa sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji ikiwa ni pamoja na rushwa na hivyo kukwamisha juhudi za kuondoa pengo la umasikini.

Mwenyekiti wa bodi ya TPSF Dkt. Reginald Mengi.

Dkt. Mengi amesema kuwa Wafanyabiashara wengi wa Tanzania wana uwezo wa kuwekeza katika sekta hizi ili kuondoa umaskini kwa Wananchi wa Tanzania na kusema viongozi wengi wamekuwa wakiwadharau na kusema hali hiyo inafanya watanzania kushindwa kujikwamua kutoka katika Umasikini.

Kwa Upande wake Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dk.Mary Nagu amesema watanzania wanao uwezo wa kushiriki katika uwekezaji wa rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na katika sekta ya mafuta na gesi

Akiongea jijini Dar es salaam Dkt.Nagu wakati akifungua mkutano mkuu wa kumi na tano wa taasisi ya sekta binafsi nchini tanzania (TPSF ) amesema ameshangazwa na kauli za kuwabeza Wafanyabiashara wazawa kuwa hawana uwezo wa kuwekeza katika rasilimali hizo.