Jumanne , 24th Dec , 2019

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Songwe, George Kyando amewaonya watu wanaokunywa Pombe kupita kiasi kwenye Mkoa huo, na kusema jeshi hilo halitawavumilia watu hao litawafikisha mahakamani.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Songwe, George Kyando.

Kamanda wa Polisi Kyando ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari, mkoani Songwe kuelekea msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

"Msimu huu wa sikukuu mtu yeyote atakaye kunywa pombe kupindukia atashughulikiwa Kama wahalifu wengine na kupelekwa mahakamani."

Kesho Disemba 25, 2019 waumini wa Dini ya Kikiristo Dunia nzima wanatarajiwa kuazimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo