Jumatano , 20th Mei , 2015

Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof. Mussa Assadi amewasilisha ripoti tano za ukaguzi wa fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30 na kuonesha upotevu wa zaidi ya bilioni 600 ya fedha za umma kutokana na ukiukwaji wa sheria.

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali Prof. Mussa Assadi

Ripoti hiyo ambayo ilitolewa kwa vyombo vya habari iliwasilishwa bungeni jana ambapo inaonesha ukaguzi ulifanywa katika Serikali kuu, serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na ufanisi wa kazi mbalimbali za serikali.

Ubadhilifu huo unaonesha umetoka katika ukiukwaji wa matumizi ya misamaha ya kodi kwa kampuni zisizostahili msamaha, malipo kwa watumishi hewa wa umma na halmashauri kutokusanya mapato kutoka kwa mawakala wa ukusanyaji wa mapato.

Akiizungumzia ripoti hiyo katika mkutano wa pamoja na CAG, Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali PAC, Bi. Amina Mwidau amesema zaidi ya bilioni 400 zimetafunwa katika kitengo cha maafa pamoja na wizara ya ujenzi.