Jumapili , 26th Nov , 2023

Kamati ya Kitaifa ya Majadiliano nchini Kenya (NADCO) imependekeza kuanzishwa kwa ofisi za Waziri Mkuu na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani

Katika taarifa ya pamoja iliyotumwa kwa vyombo vya habari timu hiyo ya wanachama 10 ilisema kuwa mazungumzo yao ya miezi 4 yalizaa azimio la kirafiki la kuunda ofisi zote mbili ili kukuza umoja wa kitaifa kati ya upinzani na serikali.

Nyadhifa hizo mbili sasa zinangoja kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa na iwapo litafanikiwa viongozi wawili ambao ni Musalia Mudavadi na kinara wa upinzani Raila Odinga, watateuliwa na Rais William Ruto. 

Aidha Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo nchini Kenya (NADCO) iliyoanzishwa Agosti 2023 ili kuondoa maswala magumu kati ya chama tawala cha Kenya Kwanza na muungano wa Azimio la Umoja imewasilisha ripoti yake
Katika ripoti hiyo kamati imependekeza kuongezwa kwa muda wa malalamiko ya urais, na tathmini ya uchaguzi wa 2022.

NADCO inapendekeza kuongezwa kwa muda ambao Mahakama ya Juu itasikiliza na kuamua ombi la kupinga uhalali wa uchaguzi wa urais kutoka siku 14 hadi 21. 

NADCO inapendekeza kuanzishwa kwa NG-CDF, Hazina ya Kitaifa ya Udhibiti wa Serikali (NGAAF), na Hazina ya Seneti ya Uangalizi katika katiba.

Kamati pia inapendekeza Mfuko wa Maendeleo ya Kata uanzishwe kwa mujibu wa sheria.
Ripoti hiyo imewasilishwa kwa uongozi wa Kenya Kwanza na Azimio la Umoja, na pia kuwasilishwa bungeni kwa mapitio zaidi.

NADCO iliongozwa na Kimani Ichung'wah wa Kenya Kwanza na Kalonzo Musyoka wa Azimio.
Wanachama wa kamati hiyo ni pamoja na Opiyo Wandayi, Eugene Wamalwa, Okon'go Omogeni na Amina Mnyazi.
Wengine ni pamoja na Araon Cheruiyot, Cecily Mbarire, Hassan Omar na Catherine