Jumatatu , 30th Mar , 2015

Wizara ya Uchukuzi nchini Tanzania, inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa reli mpya, itakayoiunganisha Tanzania na nchi za nyingine za maziwa makuu ,mradi utakaogharimu fedha za Tanzania shilingi trilioni 14.

Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta.

Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta amesema pamoja na mambo mengine, reli hiyo itasaidia kukidhi mahitaji makubwa ya ubebaji mizigi kwenda nchi jirani za Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, Burundi, na Rwanda na pia itasaidia usafirishaji wa wananchi kwenda mikoani kwa wingi na kwa kasi zaidi.

Amesema serikali imeamua kujenga reli hiyo kutokana na ile iliyopo sasa ambayo ina uwezo mdogo wa usafirishaji mizigo ambayo hata baada ya ukarabati kwa mwaka ni tani milioni tano ambazo haziwezi kukabili mahitaji ya mizigo ya kanda hiyo ambayo yatafikia tani milioni 30 mwaka 2025.

Sitta amesema Rais Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi la mradi huo, ambao ni mkubwa kuwahi kutekelezwa tangu nchi ipate uhuru, na ambao ujenzi wake utaanza Juni 30 mwaka huu kukamilika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.