Jumanne , 28th Jun , 2022

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela, ametaja majina ya viongozi wakubwa wa kwanza waliokubali kuhama katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera mkoani Tanga kuungana na wananchi wengine ambao wameshahamia.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela

Viongozi hao ni mbunge wa zamani wa jimbo la Ngorongoro Kaika Ole Telele, Diwani wa kata ya Eyasi, Augustino Lukumay, Diwani wa viti maalum wa Kata ya Eyasi Veronica Litiga pamoja na kiongozi wa kabila la Wadatoga.

RC Mongella amesema kuwa tathmini ya muendelezo wa awamu ya tatu ya  wananchi waliokubali kuhama katika eneo hilo na kwamba kundi hilo lenye kaya 25 litaanza safari Alhamisi ya wiki hii.

Mongella amesema hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika mchakato huo na kubainisha kuwa viongozi hao kwa pamoja  wamekiri kuwa wapo tayari kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera kwa lengo la kupisha shughuli za uhifadhi.