Ijumaa , 15th Apr , 2022

Uongozi wa mkoa wa Dar es salaam umetangaza kuanza zoezi la kugawa Vyandarua Bure kwa Wanafunzi 785,000 wa Shule za Msingi katika mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema zoezi la ugawaji wa Vyandarua kwenye Shule za msingi limeanza April 04 na litahitimishwa  April 28 Mwaka huu.

RC Makalla amewataka Wananchi kuwekea Mkazo mapambano dhidi ya Malaria kwa kudhibiti mazalia ya mbu huku akiwataka Wazazi kuwapeleka watoto wao wakapate chanjo ya Polio inayotaraji kuanza kutolewa April 27 mwaka huu.

Aidha RC Makalla amewataka Wananchi kusafisha maeneo yao yawe safi na salama kwakuwa ndio Msingi mzuri wa kuteketeza mazalia ya mbu na kueleza kuwa Serikali itaendelea kufanya Usafi kwenye Mitaro na Mifereji.

Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa Wazazi Wenye watoto wa Umri Chini ya miaka mitano kuwapeleka kupata chanjo ya Polio ambayo inatarajiwa kuzinduliwa April 27 na kutolewa kwa watoto 778,039 wa Mkoa wa Dar es salaam.