Jumamosi , 27th Nov , 2021

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amempongeza msemaji wa Yanga Haji Manara kwa tamko lake la kuunga mkono kampeni ya usafi ya mkoani Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

RC Makalla ameyasema hayo wakati wa kikao cha watendaji wa mitaa na Kata kilichokuwa na lengo la kujadili mikakati ya kufanikisha usafi endelevu ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa amempongeza Haji Manara na wana-Yanga wa matawi yote kwa namna walivyopanga kuhamasishana kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Aidha RC Makalla amesema Jambo la usafi ni jukumu la kila mtu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi Desemba 04, 2021, ili kushirikiana kufanya usafi wa pamoja