Jumanne , 27th Jul , 2021

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amezielekeza Halmashauri zote za mkoa huo kwa kushirikiana na TARURA zihakikishe zinaweka vibao vya 'wrong parking' kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa maegesho ili kuepuka uonevu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao kazi kati yake na wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA kilicholenga kuondoa kero ya tozo ya 'wrong parking'.

Aidha, RC Makalla amesema kikao hicho wamekubaliana tozo ya 'wrong parking' itekelezwe kwa mujibu wa sheria na kwa ambaye ataonekana alidhamiria moja kwa moja kuvunja sheria huku akisisitiza elimu iendelee kutolewa.