Jumatatu , 14th Jul , 2014

Serikali imesema inakusudia kutoa kwa wawekezaji wa Kimarekani, eneo la ranchi ya taifa la mkata lililopo wilayani kilosa mkoani Morogoro nchini Tanzania.

Waziri wa Maendeleo ya mifugo na uvuvi nchini Tanzania Dkt Titus Kamani.

Waziri wa Maendeleo ya mifugo na uvuvi Dk Titus Kamani amesema kuwapa wawekezaji ranchi hiyo kutasaidia kuiendeleza na kuwa na ufugaji wa kisasa.

Kamani amesema kuwa wawekezaji watakaoiendeleza ranchi hiyo wanakusudia kufuga kisasa hali itakayowanufaisha pia wafugaji wa maeneo jirani kujifunza na kunufaika kibiahsara kupitia sekta ya mifugo.

Ameongeza kuwa welekeo wa wizara kwa sasa kwa sekta hiyo ni kuvutia wawekezaji wakubwa wa kibiashara ili serikali ipate mitaji.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero Walace Karia ameiomba wizara ya mifugo kuhakiki mipaka ya ranchi hiyo ili kuepuka migogoro.