Ijumaa , 30th Jul , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, amemteua Rogatus Mativila, kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akichukua nafasi ya Mhandisi Patrick Mfugale, aliyefariki dunia Juni 29, 2021.

Kushoto ni Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS mteule Rogatus Mativila.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Julai 30, 2021, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, ambapo kabla ya uteuzi huo Mativila alikuwa ni Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Mbali na huyo Rais Samia pia amemteua Prof. Yunus Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo kabla ya uteuzi huo Profesa Mgaya alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR.