
Macron ameyasema hayo alipokutana na Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa mazungumzo kuhusu vita.
Trump, ambaye hakutaja hakikisho la usalama mwenyewe, alisema gharama na mzigo wa kupata amani nchini Ukraine lazima zilipwe na mataifa ya Ulaya na sio Marekani pekee.
Macron alijibu kwamba Ulaya inaelewa hitaji la kushiriki kwa usawa mzigo wa usalama, na akaongeza kuwa mazungumzo ya maadhimisho ya mwaka wa tatu wa uvamizi wa Urusi yameonyesha njia ya kusonga mbele.
Wakati wawili hao wakirushiana maneno ya makali Jumatatu nzima, baadhi ya tofauti za wazi ziliibuka kuhusu suala la kumaliza vita nchini Ukraine walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya rais wa Marekani ya Oval na kisha kufanya mkutano wa wa dakika dakika 40 na waandishi wa habari baadaye mchana.
Hata hivyo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema anatumaini kwamba wanaweza kumaliza vita hivi mwaka huu katika kumbukumbu ya mwaka wa tatu wa uvamizi kamili wa Urusi.
Lakini ameonya kuwa Ukraine inahitaji dhamana ya usalama ili kuizuia Moscow kurejea, akipendekeza uanachama wa EU na Nato kwa nchi yake utasaidia. Urusi imepinga mara kwa mara wazo la Ukraine kujiunga na Nato.