Ijumaa , 7th Mei , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kwa vitendo vya ujambazi vilivyoanza kujitokeza jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Amesema hayo leo Mei 7, 2021 alipoongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

''Nimesoma mtandaoni Dar kuna watu wanajaribu kupima kina cha maji, viujambazi vimeanza kuja juu, naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, IGP upo hapa, mitandaoni wanamtaja afande mmoja alikomesha ujambazi, wanasema Mama turudishie'' - Rais Samia Suluhu.

Aidha Rais Samia amesema huko mbeleni kwenye kujenga uchumi wa nchi atateua watu kwa kufuata welefi na si itikadi za vyama vyao.

''Katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka chama kipi yule katoka chama gani, lengo letu ni kujenga umoja wa watanzania'' - Rais Samia Suluhu.