
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Aidha Rais Samia amemteua Bwana Mavere Ali Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Tukai anachukua nafasi ya Meja Jenerali Dkt. Gabriel Saul Mhidze.
Awali Bwana Tukai alikuwa ni Kiongozi mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus kutoka Washington DC nchini Marekani imebainisha pia Rais Samia amemteua Bwana Raymond Willium Mndolwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji.