Alhamisi , 4th Feb , 2016

Rais Magufuli amewataka viongozi wa mahakama nchini kusimamia haki nchini kuhakikisha kuwa wanaendelea kuhakikisha kuwa mahakama inashiriki kikamilifu kutoa hukumu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewataka viongozi wa mahakama nchini pamoja na wanaohusika kusimamia haki nchini kuhakikisha kuwa wanaendelea kuhakikisha kuwa mahakama inashiriki kikamilifu kutoa hukumu ya haraka kwa wote wanaobainika na kesi haswa za uhujumu uchumi nchini.

Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo katika hotuba yake ya maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ametaja kuwa kucheleweshwa kwa mashauri kumeifikisha nchi pabaya ikiwa ni pamoja na kuikithiri kwa vitendo vinavyoendelea kuifanya nchi kuwa masikini.

Katika sherehe hizo Dkt. Magufuli pia ameahidi kushughulikia changamoto zote zinazoikabili mahakama nchini ikiwa ni pamoja na kuidhinisha kutolewa kwa pesa zote zilizoombwa na mahakama ili kushughulikia marekebisho ya mahakama nchini..

Wakati huo huo Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman amesema kuwa mchakato wa kuanza kwa mahakama ya kushughulia rushwa na ufisadi nchini Tanzania tayari umekwishaanza na mahakama hiyo itaanza kazi mapema mwaka huu..