Ijumaa , 6th Nov , 2015

Wakazi wa mikoa tofauti nchini Tanzania wamempongeza Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kumuomba awatumikie watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama vya kisiasa au dini.

Rais Dk. John Magufuli akiwa ameshika mkuki na ngao baada ya kukabidhiwa na wazee katika hafla ya kumuapisha iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa mkoa wa Morogoro, Geita na Mbeya wamesema wananchi wa kipato cha chini wanateseka na hali ngumu ya maisha hasa katika kutafuta huduma za afya, elimu pamoja na mambo mengine na kumuomba Rais Magufuli kutekeleza ahadi zake alizo ahidi watanzania wakati wa kampeni.

Aidha wakazi hao wamesema wanatarajia mambo makubwa kutoka kwa rais wa awamu ya tano kutokana na uzoefu wake na msimamo aliouonyesha siku zote kwa kuchukia watendaji wazembe, walarushwa pamoja na wale wanaofanya kazi kwa mazoea pamoja na kuwashughulikia mafisadi kwani watanzainia wanahitaji kuondoa matabaka ya wenye nacho na wasiokuwa nacho

Aidha wakazi hao wakiwemo wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga wamesema akitekeleza suala la ushuru ambao umekuwa kero kwao itakua rahisi kwa wao kukuza mitaji yao.