Rais Lungu akiagwa katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka
Rais Lungu ameysema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam na bandari kavu inayohifadhi na kusafirisha mizigo kutoka na kuingiza Zambia.
Amesema watendaji waache kufanya kazi kwa mazoea hasa kwa kuangalia mlengo wa vyama vya siasa kwani kwa kufanya hivyo wanawanyima haki watumiaji wa bandari hiyo ambayo inategemewa katika kuingiza kipato cha nchi ya Zambia na Tanzania.

Rais Lungu akiwa ziarani TAZARA
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Zambia haina budi kwa wananchi wake kuendeleza ushirikiano huo kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia malengo waliojiwekea na ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Zambia na ushirikiano huu utazidi mara dufu.





