Kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza jopo la viongozi wakiwemo marais wastaafu katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine yatakayofanyika wilayani Monduli mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ndiye aliyekuwa mwenyeji wa ugeni uliohudhuria maadhimisho hayo yaliyoshirikisha baadhi ya viongozi walioshiriki ni pamoja na Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, mjane wa baba wa taifa mama Maria Nyerere, watendaji mbali mbali wa serikali na wananchi kwa ujumla.
Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zimefanyika kwa lengo la kumuenzi kiongozi huyo shujaa aliyepigania wanyonge katika kipindi chote cha maisha yake na kwamba makundi mbalimbali yamejitokeza kushiriki kufikisha ujumbe unaolenga kuenzi na kuendeleza yote aliyaanzisha hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki mwaka 1984 kwa ajali ya gari.
Rais Kikwete amesema Serikali itaendelea kuyaenzi yote ambayo Hayati Sokoine aliyapigania ikiwa ni pamoja na uadilifu pamoja vita dhidi ya rushwa.
Baadhi ya wananchi maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wameyaelezea madhimisho hayo kwa mitazamo tofauti sambamba na kutoa maoni yao jinsi watanzania wanavyoweza kumuenzi kiongozi huyo.
Maadhimisho hayo yamefanyika nyumbani kwa familia ya hayati Sokoine kata ya Monduli juu Wilayani Monduli.