Jumatano , 5th Jan , 2022

Watu watano wakiwemo watoto wanne waliokuwa wakicheza chini ya mti wakati mvua ikinyesha wamepoteza maisha kwa kupigwa na radi katika Kijiji cha Kibuye, Kata ya Kumsenga wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

Radi

 

 

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi  mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, na kusema tukio hilo limetokea jana Januari 4, 2022, na kwamba waliopoteza maisha ni watoto wanne kutoka familia tofauti na mwingine akipigwa na radi na kupoteza maisha wakati akiwa anaendelea kulima shambani.

Aidha, Kamanda Manyama ametoa tahadhari kwa wananchi mkoani Kigoma hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua ili kuepusha madhara zaidi.