Jumatatu , 18th Oct , 2021

Radi iliyoambatana na mvua imeuwa ng'ombe 15 usiku wa kuamkia leo Oktoba 18, 2021, katika Kijiji cha Zaire kilichopo Kata ya Ikomwa, Manispaa ya Tabora, ambapo ndani ya Zizi kulikuwa na ng'ombe zaidi ya 30

Ng'ombe waliokufa baada ya kupigwa na radi

Serikali ya wilaya ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda, imefika katika eneo la tukio kwa lengo la kuwapa pole wanafamilia.

Kufuatia hali hiyo serikali imeahidi kufanya tathmini kwa ajili ya kumshika mkono Homano Lugwesa, ambaye ni mmiliki wa ng'ombe hao.